1 Kings 15:1-6

Abiya Mfalme Wa Yuda

(2 Nyakati 13:1–14:1)

1Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yeroboamu mwana wa Nebati, Abiya akawa mfalme wa Yuda, 2 anaye akatawala huko Yerusalemu miaka mitatu. Mama yake aliitwa Maaka binti Abishalomu.
Yaani Absalomu, maana yake Baba wa amani.

3 cAlitenda dhambi zote baba yake alizotenda kabla yake; moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana Mwenyezi Mungu wake kama moyo wa Daudi baba yake ulivyokuwa. 4 dPamoja na hayo, kwa ajili ya Daudi, Bwana Mwenyezi Mungu wake akampa taa katika Yerusalemu kwa kumwinua mwana atawale badala yake na kwa kuifanya Yerusalemu kuwa imara. 5 eKwa kuwa Daudi alifanya yaliyo mema machoni pa Bwana na hakushindwa kushika maagizo yote ya Bwana siku zote za uhai wake, isipokuwa katika habari ya Uria, Mhiti.

6 fKulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu wakati wote wa maisha ya Abiya.
Copyright information for SwhKC